Chukueni tahadhari dhidi ya Magonjwa ya mlipuko

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wananchi Mji mdogo wa Katesh Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara na Watanzania kwa ujumla kuendelea kuchukua tahadhari za magonjwa ya mlipuko kwa kuchukua hatua za matumizi ya maji safi na salama.

Dkt. Samia ametoa wito huo leo Disemba 7 ,2023 wakati akizungumza na wananchi mji mdogo wa Katesh Wilayani Hanang Mkoa Manyara baada ya Disemba 3, 2023 kukumbwa na maafa ya mafuriko yaliyosababisha maporomoko ya udongo kutoka mlima Katesh na kusababisha madhara makubwa ikiwemo majeruhi,vifo na upotevu wa mali.


“Jambo kama hili linapotokea huwa yanatokea magonjwa ya mlipuko ,niwaombe wananchi wachukue hatua stahiki za kuzingatia kanuni za afya pindi wanapotumia maji wazingatie kuepuka magonjwa ya mlipuko ikiwemo kuhara “amesema.

Aidha, Rais Samia ametoa maagizo kwa Wizara ya Afya kuhakikisha elimu na ufuatiliaji kwa kina inatolewa kwa wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *