Waziri wa masuala ya haki nchini Senegal Aissata Tall Sall ametangaza kuachiwa huru kwa karibia waandamanaji 400 wa kisiasa kutoka jela.
Waandamanaji hao walikamatwa na kufungwa gerezani wakati wa maandamano ya mwezi Machi mwaka wa 2021 na mwezi Juni 2023.
Maandamano ya kisiasa nchini Senegal yamekuwa yakifuatiwa na ripoti za watu kukamatwa na polisi, vifo pia vikithibitishwa kutokea.
Hivi karibuni, watu watatu walithibitishwa kufariki wakati wa maandamano ya kupinga kuhairishwa kwa uchaguzi mkuu wa tarehe 25 ya mwezi Februari.
Baada ya tangazo hilo, kiongozi huyo amesema uchunguzi unaendelea kubaini waliokuwa nyuma ya maandamano ya vurugu.