Waziri Mkuu DRC Congo ajiuzulu

Waziri Mkuu wa DR Congo, Jean-Michel Sama Lukonde ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Uwaziri Mkuu, nafasi aliyoitumia toka Fenruari mwaka 2021 akichukua nafasi ya Sylvestre Ilunkamba aliyejiuzulu baada ya kupigiwa kura ya kutokua na imani naye.

Ofisi ya Rais katika taarifa yake imesema kujiuzulu kwa Lukonde kumesababisha kuvunjwa kwa Serikali nzima, Waziri Mkuu huyo aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Rais Felix Tshisekedi, Hata hivyo Rais ameiomba Serikali (Ya Lukonde) kuendelea kushughulikia serikali mpaka itakapoundwa serikali mpya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *