Jambo La Leo

Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Ummy aridhishwa na wahudumu wa afya Shinyanga

Waziri Wa Afya, Ummy Mwalimu Ameelezea Kuridhishwa Na Ubora Wa Huduma Zinazotolewa Katika Hospitali Ya Rufaa Ya Mkoa Wa Shinyanga Kwa Kuwezesha Utoaji Wa Huduma Za Afya Kwa Asilimia 100 Na Kutoa Pongezi Kwa Wafanyakazi Wa Hospitali Hiyo.

Ametoa Pongezi Hizo Leo 13 Julai 2023 Baada Ya Kutembelea Hospitali Hiyo Na Kujionea Namna Huduma Zinavyotolewa Na Kuahidi Kwamba Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Ataendelea Kuchukua Hatua Mbalimbali Ikiwemo Kutoa Fedha Kwa ajili Ya Kukamilisha Maeneo Ambayo Hayajakamilika Katika Hospitali Hiyo.

Aidha Amewasisitiza Watumishi Wa Sekta Ya Afya Nchini Kuzingatia Utoaji Wa Huduma Kwa Viwango Kwa Kuboresha Zaidi Maeneo Mbalimbali Ikiwa Ni Pamoja Na Muda Wanaotumia Wagonjwa Kupata Huduma,Upatikanaji Wa Vipimo Na Dawa Ili Kuwawezesha Wagonjwa Kuendelea Na Shughuli Zao Baada Ya Kupatiwa Matibabu.

Waziri Ummy Pia Ameuagiza Uongozi Wa Hospitali Ya Mkoa Wa Shinyanga Kuhakikisha Huduma Zote Za Vipimo Vya Kimaabara Zinazopaswa Kutolewa Katika Hospitali Hiyo zinapatikana Ili Kuendana Na Hadhi Ya Hospitali Ya Rufaa pamoja Na Matumizi Mazuri Ya Lugha Kwa Wagonjwa Na Kuwahudumia Kwa Upendo.

Awali Akizungumza Kwa Niaba Ya Mkuu Wa Mkoa Kabla Ya Kumkaribisha Waziri Ummy Mwalimu, Mkuu Wa Wilaya Ya Shinyanga Johari Samizi Amesema Kwamba Juhudi Za Rais Dkt. Samia Katika Kuhakikisha Huduma Bora Za Afya Zinapatikana Kwa Watanzania Wote Zinaonekana Wazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *