Naibu Katibu Wizara ya Afya Dkt. Magembe amewahimiza wananchi kuendelea kutoa mrejesho wa huduma wanazopatiwa kupitia ujumbe mfupi wa simu,masanduku ya maoni na kupiga simu kwa kutumia namba za viongozi wa hospitali, Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri, mitandao ya kijamii ya Wizara pamoja na namba ya Wizara 199 au njia yoyote watakayoona ni ya haraka kufikisha ujumbe mahali husika.
Dkt. Magembe amesema hayo alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tumbi Pwani kuona hali ya utoaji huduma za matibabu ambapo alizungumza na wananchi Aidha, ametumia muda huo kuwakumbusha watumishi wa afya kuwa tayari kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi kwa wakati.
Dkt. Magembe amepongeza uongozi wa Hospitali ya Tumbi kwa kutoa huduma bora za matibabu kwa wananchi na kuwataka watumishi wa afya kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kwa kuzingatia maadili ya taaluma zao.