Maaskofu 14 wa kanisa katoliki wametiwa mbaroni, kufuatia msako mkali dhidi ya kanisa katoliki nchini nicaragua hatua ambayo imesababisha Papa Francis kutoa wito wa kufanyika mazungumzo.

Kwa mujibu wa orodha iliyoandaliwa na mtaalamu wa masuala ya kanisa wa Nicaragua Martha Molina, ambaye anaishi uhamishini nchini Marekani amesema Askofu Gustavo Sandino kutoka eneo la kaskazini la Jinotega alikamatwa usiku wa mkesha wa mwaka mpya.
Kuzuiliwa kwake ni kutokana na mkasa wa hivi karibuni katika wimbi la kamatakamata la Rais Daniel Ortega wa mrengo wa kushoto, ambalo lilianza Desemba 20 kwa kumwekwa kizuizini Askofu Isidoro Mora.
Uhusiano kati ya Kanisa na serikali ya Ortega ulidorora wakati wa maandamano ya kupinga mageuzi ya hifadhi ya jamii mwaka 2018, ambayo Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa yalisababisha vifo vya takriban watu 300.