Nyota wa muziki wa pop kutoka Marekani Taylor Swift ametangazwa rasmi kuwa ni bilionea, hii ni kwa mujibu wa mtandao wa Bloomberg.
Swift anatajwa kuwa na utajiri wa dola bilioni 1.1, na hii ni kutokana na ziara ya Eras ambayo imemsaidia kukuza uchumi.