Kamati ya Mashindano ya Kombe la Mapinduzi imetangaza makundi matatu huku kila kundi likiwa na timu 4 kwenye timu 12 zitakoshiriki Mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza rasmi Disemba 28, 2023 na kumalizika Januari 13, 2024 kwenye Uwanja wa Amaan.
Kundi ‘A’
Mlandege FC (Zanzibar), Azam FC (Tanzania), Chipukizi (Zanzibar), URA (Uganda)
Kundi ‘B’
Simba SC (Tanzania), Jamhuri (Zanzibar), APR (Rwanda) na Singida Fountain Gate (Tanzania)
Kundi ‘C’
Yanga SC (Tanzania), Bandari (Kenya), KVZ (Zanzibar), na Vital’o (Burundi).