Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Rais Samia Avunja Bodi Ya TANESCO

Kufuatia Balozi Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kuteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uganda tarehe 18 Desemba, 2023, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameivunja Bodi hiyo na amemteua Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Simuli.

Dkt. Nyansaho ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Azania. Uteuzi huu unaanza mara moja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *