Jambo La Leo

Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Wawekezaji watengewe maeneo

Wakurugenzi katika halmashuri zote za mkoa wa Shinyanga wametakiwa kutenga maeneo ya uwekezaji na kuhakikisha kuwa, wananchi wanaomiliki maeneo husika wanalipwa fidia zao kikamilifu pale wanapotakiwa kupisha maeneo ya uwekezaji ili kupunguza malalamiko toka kwa wananchi.

Agizo hilo limetolewa leo Disemba 19, 2023 na mkuu wa mkoa wa Shinyanga @christinamndeme18 wakati akifungua kikao cha baraza la biashara la mkoa kilichofanyika leo katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa huku akisema mkoa huo una maeneo mengi ya uwekezaji katika eneo la madini kilimo mifugo viwanda elimu nishati utalii na mawasiliano ambapo amewtaka wakwekezaji kujitokeza kuwekeza katika maeneo hayo.

Aidha Mndeme amezitaka pia taasisi za umma ambazo ni Ruwasa, Shuwasa, Kashuwasa, Kuwasa, Tanesco, Tanroad na Tarura kuongeza kasi ya kuweka miundo mbinu wezeshi katika maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji katika kila halimashauri zilizopo katika mkoa wa Shinyanga.

Vikao vya baraza la biashara vilianzishwa kwa mujibu wa waraka namba moja wa raisi wa mwaka 2001 dhumuni kuu likiwa ni kuweka mfumo rasimi wa kuwakutanisha viongozi wa serikali na sekta binafsi ili kujadiliana jinsi ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuinua sekta binafsi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *