Mamalaka ya maji safi na usafi wa mazingira mkoa wa shinyanga (Shuwasa) imepunguza upotevu wa maji kutoka asilimia 26 mwezi Juni mwaka 2021 hadi asilimia 20 mwezi June mwaka 2023.
Mkurugenzi mtendaji mamalaka ya maji safi na usafi wa mazingira mkoa wa Shinyanga mhandisi Yusuph Katopola amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuongeza kuwa mauzo ya maji yameongeza kufikia aslimia 27.8 kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ikilinganishwa na mwaka wa fedha 2021.
Aidha mhandisi Katopola amesema wapo katika utekelezaji wa miradi takribani 10 ya mendeleo katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Shinyanga inayogharimu kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 5 itakayowanufaisha wananchi wapatao laki 1 na elfu 16 ambapo miradi 7 kati ya hiyo imeshaanza huduma na mitatu iliyosalia ikitarajiwa kukamilika february mwaka huu.
Pamoja na hayo mhandisi Katopola amesema watakopa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo mtambo wa kuchakata maji taka na ujenzi wa vyoo kwa maeneo 36 ya shule na vituo vya afya na mabasi katika halimashauri na manispaa ya Shinyanga