Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Serikali yasisitiza malalamiko rushwa ya ngono kwa wanafunzi yaripotiwe haraka

Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, imesema malalamiko yoyote ya rushwa hasa ya ngono kwa wanafunzi yaripotiwe haraka ili hatua zichukuliwe kwa ajili ya kukomesha vitendo hivyo.

Kauli ya serikali imetolewa na Waziri wa Elimu, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, wakati wa maswali na majibu Bungeni Jijini Dodoma, akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Nusrat Anje,ambaye ameuliza kwa nini serikali isione umuhimu wa kuhamisha mamlaka ya usimamizi wa mitihani vyuo vikuu kuwa chini ya usimamizi wa wahadhiri ili kuondoa mianya ya rushwa ya ngono kwa wahadhiri.

Waziri mkenda amewataka wazazi na nawanachi kwa ujumla kutoa taarifa za kweli kuhusiana na vitendo vya rushwa kwa wanafunzi ili kupatikana kwa haki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *