Jumuiya ya kimaendeleo ya nchi za Magharibi, ECOWAS imesema ipo tayari kwa mazungumzo ya kupata mwafaka baada ya nchi tatu wanachama, Burkina Faso, Mali Na Niger kutangaza kujiondoa kwenye muungano huo.
ECOWAS imesema nchi hizo tatu zilikuwa wanachama muhimu kwenye jumuiya hivyo ilikuwa imejitolea kupata suluhisho ya kisiasa kutatau mzozo kati yake na nchi hizo,ingawaje ECOWAS imesisitiza haijapata taarifa rasmi ya nchi hizo kusitisha uanachama wao.
Mataifa hayo matatu ambayo ni wanachama wa ECOWAS tangu 1975 zimekuwa na uhusiano baridi baada ya kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na jumuiya hiyo baada ya mapinduzi.