Rais Samia ni mwanamke mwenye ushawishi na Nguvu Duniani

Jarida la Forbes 2023 limemtaja Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt Samia Suluhu Hassan kama wanawake mwenye ushawishi na nguvu zaidi Duniani.

Jarida hilo limetoa orodha ya wanawake 100 ambapo Rais Samia anashika nafasi ya 93 kutoka nafasi ya 95 mwaka 2022.

Rais Samia amekuwa Rais wa sita wa Tanzania na kiongozi wa kwanza mwanamke mnamo Machi 2021, kufuatia kifo cha Rais John Magufuli.

Alipanda wadhifa huo kutoka kwa Makamu wa Rais, ambapo alichaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo 2015.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *