BODABODA UNDENI VIKUNDI VYA KUPATA MKOPO – DC MASWA.

Mkuu wa wilaya ya Maswa Dkt Vicent Naano amewataka vijana wanaojihusisha na biashara ya usafirishaji maarufu bodaboda kuunda vikundi vitakavyowawezesha kupata mikopo ya serikali zikiwemo boda boda na hatimaye wazidi kujikwamua kiuchumi.

Naano ameyasema hayo alipowatembelea vijana hao katika baadhi ya vituo vyao wilayani humo lengo likiwa ni kusikiliza changamoto wanazozipitia katika shughuli zao za kila siku na kuwasisitiza kuweka akiba ya mali zao kwani kazi wanayofanya hawatodumu katika Maisha yote.

“Hii ni kazi kama kazi zingine lakini si kazi ambayo utaweza kudumu nayo hadi uzeeni,kwa sasa undeni vikundi mfahamike mpate mikopo ya serikali na hata kupewa bodaboda lakini msiache kujiwekea akiba na kutunza mali zisizo hamishika hii itakuwa faida kwenu hapo baadae” amesema DC Naano

Sambamba na hilo Naano amewataka Maafisa hao kuendelea kutoa ushirikiano na jeshi la polisi ili kuweza kuwabaini wahalifu ambao wajipachika miongoni mwao na kutaka kuchafua sifa za maafisa hao kwa kudhuru wananchi.

“kuna watu wenye nia ovu wanajipachika miongoni mwenu na wengine mitaan tunawajua niombe ushirikiano wenu kwa jeshi la polisi ili kuweza kuwabaini watu hawa wanaodhuru wananchi” ameongeza DC Naano.

Naye mkuu wa usalama barabarani wilayani humo Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi James Nyorobi amewataka maafisa hao kuzingatia kanuni na sheria za barabarani ikiwa ni pamoja na kutokupakiza abiria zaidi ya mmoja katika vyombo vyao pamoja na kuvaa kofia ngumu ili kujiweka salama wao na abiria wao.

“Ninawaasa mambo makuu matatu kwanza ni kuzingatia sheria kwa kufuata mataa,kuacha ulevi ,kuvaa kofia ngumu japokuwa suala la kufuata mataa limekuwa mtambuka hamzifuati ndiyo maana tunaendelea kuwapa elimu ili mbadilike na kuendana na wakati mjue ni namna gani ya kuzitumia hizi taa ambazo zimewekwa kwa gharama kubwa kwa ajili yanu”Amesema Mkaguzi James Nyorobi.

Akizungumza kwa niaba ya maafisa hao Amos Charles amekiri kuwa  baadhi ya maafisa hao hawajui namna ya kutumia taa za barabarabi hali inayosababisha kutokea kwa migongano kati yao na watumiaji wengine wa barabara.

“unafika kwenye mataa lakini hujui ni wakati gani unatakiwa uvuke wewe na wakai gani avuke mtembea kwa miguu mwisho wa siku muda wa mtembea kwa miguu unavuka wewe muda wa wewe kuvuka anavuka mtembea kwa miguu kwa hiyo mtupe elimu hatuzijui hizi taa matumizi yake” amesema Amos.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *