Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Ajali ya Hiace Bukoba vifo vimefika sita

Mkuu wa Wilaya Bukoba, Erasto Sima amesema kuwa vifo vya watu waliopata ajali ya gari iliyohusisha gari aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajili T.339 DBV imeongezeka kutoka watu wanne hadi sita jioni ya leo.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari baada ya kuwajulia hali majeruhi wanaoendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kagera Bukoba, mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa watu hao wamefariki wakiwa wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali hiyo.

Sima amesema kuwa hadi sasa majeruhi 19 wanaendelea na matibabu ambapo amewashukuru watoa huduma wa hospitali ya halmashauri ya wilaya Bukoba pamoja na hospital ya rufaa kwa namna wanavyoendelea kutoa huduma kwa majeruhi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *