Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Rais Samia atia neno Panga pangua ya mawaziri

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaapisha Viongozi wateule Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar leo September 01,2023 ambapo amesema mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri na Makatibu Wakuu aliyoyafanya sio adhabu bali ni mabadiliko ya kawaida ya kuimarisha maeneo ya utendaji kazi.

“Mabadiliko haya sio adhabu, ni mabadiliko ya kawaida ya kuimarisha maeneo yetu, natarajia commitment na utumishi, sisi ni Watumishi wa Watu sasa kuna mwingine akipata uteuzi anajiona eeh atanijua Mimi ni nani, sisi ni Watumishi wa Watu, katika utumishi mahusiano ni jambo zuri sana, ukijipandisha unataka kukaribia Mbinguni kwamba umepata uteuzi wewe nani wewe nani hutotumikia Watu”

“Mabadiliko haya ni adjustment , maendeleo lazima yawe na bandika bandua, kaza nati fungua, toa nati hii weka hapa ndio maana ya mabadiliko haya lakini tukikaa wenyewe (Kwenye kikao kazi) nitawaeleza kiundani”- Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *