Rais Samia Aelezea Mafanikio ya Ushirikiano

Mapema leo jijini Nairobi nchini Kenya akihutubia katika Mkutano wa Shirikisho la Maendeleo la Kimataifa (IDA), Rais.Dkt Samia Suluhu Hassan amesema kuwa pamoja na miradi mingine, kwa ushirikiano na IDA Tanzania imeweza pia kuboresha eneo la afya ya mama na mtoto tukiwa na moja ya mifumo bora zaidi kwa ukanda wa Afrika,kuimarisha usambazaji umeme vijijini, eneo ambalo pia Tanzania ni moja ya nchi bora zaidi kwenye ukanda huu wa bara la Afrika.

Aidha Rais Samia amesema pia kama nchi tumefanikiwa kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama, na kuanza kwa miradi mikubwa ya kudhibiti mafuriko hasa katika Jiji la Dar es Salaam ikiwemo mpango wa uboreshaji wa Bonde la Mto Msimbazi ili kudhibiti mafuriko ya mara kwa mara (Msimbazi Basin Development Project).

Pia kupitia hotuba yake Rais.Dkt Samia amesisitiza kuwa na sera bora za kifedha toka mashirika ya kimataifa kwa bara la Afrika, zenye masharti na gharama nafuu, zinazotazama kuongeza uwekezaji katika kukuza rasilimali watu na teknolojia na kujikita zaidi katika kukuza uwezo wa kuongeza idadi ya mipango inayotekelezwa kati yake na nchi washiriki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *