TAKUKURU YAOKOA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 700 MWANZA

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na wadau wa kamati ya haki ya wilaya ya Nyamagana wameokoa zaidi ya shilingi milioni 700 kwenye utoaji wa mikopo ya asilimia 10 za mapato ya ndani fedha ambazo zilikua zinatarajia kutolewa kwa vikundi visivyokidhi vigezo

Hayo yameelezwa na kaimu mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa mkoa wa Mwanza, Protas Henry ambae amesema katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi januari hadi machi mwaka huu wamefanya uhakiki katika katika maeneo mbalimbali ikiwemo atika zoezi la utoaji wa mikopo ya asilimia kumi za mapato ya ndani kwa mwaka 2024/25 na kufanikiwa kuokoa jumla ya shilingi Milioni 787,592,708 ambazo zilitarajia kutolewa kwa jumla ya vikundi 41 ambavyo vilikua havijakidhi vigezo na vilibainika na makosa mbalimbali ikiwemo kuomba mikopo kwenye miradi hewa pamoja na kuwasilisha vielelezo vya kughushi.

“Katika uhakiki huo vikundi 41 havikukidhi vigezo ambavyo mikopo yake ilikuwa na thamani ya zaidi ya Sh. Millioni 700. Vikundi hivyo vilibainika na makosa mbalimbali ikiwemo kuomba mkopo kwa miradi hewa, kuwasilisha kwa kamati vielelezo vya kugushi mfano: Profoma invoice na mikataba ya uongo ya maeneo ya kufanyia biashara, kuwasilisha bei za juu za vifaa kuliko bei ya soko, kutokuwa na maeneo ya kufanyia biashara na kuomba mkopo kwa ajili ya mradi wa mtu binafsi au familia.”

Katika hatua nyingine Protas amesema katika zoezi hilo la utoaji mikopo jumla ya vikundi 87 vilikidhi vigezo kati ya vikundi mia moja na ishirini na nane vilivyoomba mikopo.

Aidha Protas amesema kwa upande wa ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo Takukuru imeokoa kiasi Milioni 17,372,708.26 fedha ambazo ni malipo ya kodi ya zuio kutokana na utekelezaji wa miradi kwenye Sekta ya Elimu.

“Fedha hizo ni za malipo ya kodi ya zuio kutokana na utekelezaji wa miradi kwenye Sekta ya Elimu iliyofuatiliwa katika kipindi tajwa hapo juu,” amesema.

Pia amesema kwa upande wa uchunguzi na Mashtaka Takukuru Mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza imekoa Milioni 64,000,000 ambazo ni malipo ya wachimbaji wadogo wa madini kutoka kwa Mwekezaji wa Kampuni ya LHT Mining Co.Ltd.

” Kampuni ya LHT Mining Co. Ltd ilivunja Mkataba wa makubaliano baina yake na kikundi cha Nyabayombe bila ya kufuata taratibu za mkataba ikiwemo kutokuhusishwa kwa wanakikundi hali ambayo ilipelekea wamiliki wa maduara kutopata stahiki zao. Hivyo, Takukuru baada kuchunguza kwa kina imefanikiwa kuokoa kiasi hicho cha Shs. 64,000,000/= ambacho kimesaidia wamiliki hao wa maduara kulipwa stahiki zao,”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *