Safari ya Ramadhan Brothers Mlima Kilimanjaro Inaendelea

Mabingwa wa American Got Talent 2024, Ramadhan Brother (Fadhil Ramadhan na Ibrahim Ramadhan) kutoka Tanzania wanaendelea na safari yao ya kupanda mlima Kilimanjaro waliyoianza siku ya jana Aprili 29,2024 kwa lengo la kutangaza utalii wa ndani pamoja na kuhamasisha Watanzania wote kupigia kura Hifadhi za Taifa Serengeti na Mlima Kilimanjaro katika tuzo za World Travel Awards


Awali Ramadhan Brothers walikabidhiwa bendera ya Tanzania kwa lengo la kuifikisha kileleni na pia katika safari hiyo wamebeba na tuzo yao ya AGT ambayo wanatarajia kufika nayo kileleni kwa lengo la kuongeza hamasa kwa watu wa ndani na nje nchi kuupanda Mlima Kilimanjaro.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *