
Vita ni vita muraa!, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla mapema leo alitoa motisha ya Shilingi Milioni 5 Kwa Wachezaji na benchi la ufundi wa Pamba Jiji FC kuelekea mechi yao dhidi ya Biashara United FC Jumapili hii uwanja Nyamagana, Mwanza.
Lakini Mkuu wa Mkoa Mara Mhe. Said Mtanda nae amejibu mapigo kwa kuahidi nonge nono kwa timu ya Biashara United FC iwapo itaifunga Pamba Jiji FC, licha ya kutoweka wazi kiasi cha fedha, pia atapambana na wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Mara, kwenda kuishuhudia mechi hiyo.