Watu wawili wamefariki dunia na wengine wawili wamejeruhiwa baada ya moja ya gari katika Msafara wa Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Biteko kupata ajali katikati ya eneo la Mamboleo na Kwafungo Mkoani Tanga wakati Dkt. Biteko alipokuwa anaenda kukagua bwawa la uzalishaji umeme Hale Power Station leo Januari 26, 2024.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Bombo mkoa wa Tanga Frank Shega amethibitisha kupokea Kwa Majeruhi wanne kutoka Hospitali ya Muheza waliopata ajali katika Msafara wa Naibu Waziri mkuu na waziri wa Nishati Dkt Dotto Biteko ambapo amesema kati ya majeruhi hao, wawili wamepoteza Maisha kutokana na kuwa katika hali mbaya.