Rais Samia ajibu ombi la Salama Jabir la kufanya naye mahojiano

Kupitia ukurasa wa mitandao wa X (Zamani Twitter) Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan amejibu comment ya Mtangazaji Samala Jabir ya  kulifanyia kazi ombi lake la kumfanyia mahojiano na Mtangazaji huyo.



Rais amemjibu kwamba Mungu akijalia ombi lake litafanyiwa kazi kwenye birthday ya mwaka kesho kwani mwaka huu Wadogo zake Salama na Wajukuu wameshamuwahi na hivyo amemualika kwenda kula keki kwenye birthday hii ya mwaka huu akisema “lakini ya mwaka huu karibu japo ule keki kwa niaba ya wote walionitumia salamu za kheri”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *