Katika mahojiano aliyofanya Oga Obina TV ya nchini Kenya ,Staa wa muziki kutoka nchini humo Otile Brown amesema Ukanda wa Afrika Mashariki hakuna msanii wa Kimataifa

Otile amesisitiza hilo licha ya mtangazaji kumtaja Diamond Platnumz, lakini mkali huyo wa R&B aliishia kumtolea mfano msanii wa Nigeria, Ruger jinsi alivyopambana na kuweza kupenya kimataifa ndani ya muda mfupi