Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Novak Djokovic atupwa nje ya Australian Open na kijana mdogo

Kinara wa mataji makubwa ya Tenisi (Grand Slam) upande wa wanaume Duniani, Novak Djokovic (36), ametupwa nje ya michuano ya wazi ya Australia (Australian Open), akicheza dhidi ya kijana mdogo raia wa Italy Jannik Sinner (22).

Hii ni mara ya kwanza tangu mwaka 2018 Djokovic anapoteza kwenye Australian Open, ambapo pia ni mara ya kwanza kwa Sinner kutinga fainali ya michuano mikubwa ya Tenisi Duniani.

Djokovic alikuwa akifukuzia rekodi ya kuongeza mataji 11 na kubeba taji la 25 la Grand Slam ili kuipiku rekodi ya Margaret Court ambaye anazo 24, ambapo hata hivyo amekwama.

Sinner atacheza fainali Jumapili hii na mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Daniil Medvedev na Alexander Zverev.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *