Aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Ibrahim Msabaha (72) amefariki dunia leo Jumanne, Februari 13, 2024 wakati akiwa njiani kutoka nyumbani kwake, Masaki kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Jijini Dar es Salaam.
Taarifa zimeeleza kuwa Dkt. Msabaha amefariki dunia akiwa njiani akipelekwa Hospitali ya Muhimbili baada ya hali yake kubadilika ghafla ikiwa ni siku chache tangu atoke Hospitali alikokuwa amelazwa.
Aidha, Dkt. Msabaha amewahi kuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Kibaha, mkoani Pwani kupitia Chama cha Mapinduzi