Wapelelezi nchini Kenya wanachunguza hali ya kiufundi ya gari alilokuwa akiendesha Kelvin Kiptum na kocha wake raia wa Rwanda Gervais Hazikimana waliokuwa na mtu mwingine wa tatu kabla ya kupata ajali mbaya ya barabarani kwenye barabara ya Eldoret Eldama Ravine Februari 11 2024.
Wachunguzi hao wanasema bado ni mapema kueleza ni nini kilitokea kabla ya ajali hiyo iliogharimu maisha ya mwanaridha huyo aliyekuwa na kocha wake raia wa rwanda pamoja na mwanamke mmoja wakitokea eldoret kuelekea eldama ravine.
Mbali na uchunguzi wa kiufundi, wapelelezi pia wanachunguza mwili wa mwanariadha huyo pamoja na kocha wake lakini pia kupata ushuhuda wa waliotokea katika êneo la tukio baada tu ya kutokea kwa ajali.