Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mwana FA Aingilia kati Sakata La Kayumba na Director Mzava

Saa chache baada msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya (Bongo Fleva) Kayumba kuandika kwenye mtandao wa kijamii kulalamika juu ya kudhulumiwa pesa zake na Director Elly Mzava wa Next Level, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma (Mwana FA) ameliingilia sakata hilo.

Kayumba kupitia instagram ameandika ‘Napenda Kutoa Shukrani kwa Wizara @wizara_sanaatz Kwa Support na Msaada Niliyopata Kutokana Na Changamoto Niliyopitia. Siku ya Leo nimepata wito kutoka Kwa Mh.Naibu Waziri mwanafa kupitia wizara ya Utamaduni ,Sanaa na Michezo Ambapo tumeweza Kuzungumza na Kupata Muhafaka wa namna nzuri yakufanikisha
kupata Haki yangu’

‘Nashukuru Shabiki zangu Na Wote Mnaozidi Kutetea Industry Ya #BongoFleva Kwa Ujumla,
Mpaka sasa Mambo yote tumeikabidhi’ – Kayumba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *