Jambo La Leo

Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mtu na kaka yake wamekamatwa wakitorosha madini

Watu wawili ambao ni kaka na mdogo wake wamekamatwa wakitorosha vipande 28 vya madini ya dhahabu katika Mkoa wa madini Mbeya, yenye uzito wa kilo 1.083 vikiwa na thamani ya zaidi ya milioni 140.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera, amesema watuhumiwa hao wamekamatwa usiku wa kuamkia Novemba 11 ,2023 ambapo watuhumiwa hao walikuwa na nia ya kuipotezea serikali mapato ya zaidi ya millioni mbili na laki nane.

Kwa upande wake afisa madini mkazi wa mkoa wa madini Mbeya Mhandisi Oscar Kalowa, ameeleza hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa dhidi ya watuhumiwa wa utoroshaji wa madini ikiwemo madini na Mali zilizo husika kutaifishwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *