Wanaotakiwa kuanza Elimu ya Msingi waandikishwe

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Deogratius Ndejembi amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuhakikisha uandikishaji wa wanafunzi wa awali na darasa la kwanza unafanyika kikamilifu.

Ndejembi ametoa maelekezo hayo leo Novemba 13 2023 wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watendaji katika halmashauri hiyo.

Ndejembi amesema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule za msingi na za awali hivyo uandikishaji ni lazima uendane na jitihada zilizofanywa na mheshimiwa Rais.

“Kazi kubwa ya ujenzi na ukarabati wa madarasa katika shule za msingi na awali imefanyika, hivyo watendaji wa Serikali tunapaswa kuhakikisha watoto wote wanaotakiwa kuanza elimu ya awali na msingi wanaandikishwa ili watumie miundombinu iliyonjengwa na Rais Samia.”

Aidha, Ndejembi ametoa wito kwa Halmashauri zote ambazo hazijakamilisha ujenzi wa miundombinu ya shule za msingi na awali na ambazo hazijakamilisha usajili wa shule kuhakikisha wanakamilisha haraka iwezekanavyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *