Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ( DCEA) imesema Watanzania 1200 wamekamatwa katika nchi mbalimbali wakituhumiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Aidha imesema hakuna takwimu rasmi za Watanzania ambao wamenyongwa kwa sababu ya kukamatwa na dawa za kulevya huku ikitumia nafasi hiyo kueleza kwamba nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania zinatumika kama mapito ya dawa za kulevya.
Akizungumza mbele ya wahariri wa vyombo vya habari wakati wa semina iliyoandaliwa na DCEA yenye lengo la kuwajengea uelewa Wahariri na kuelezea majukumu yake, Kamishina wa Kinga na Tiba wa mamlaka hiyo Dk.Peter Mfisi amefafanua kumewepo na taarifa za watanzania kukamatwa nchi mbalimbali wakituhumiwa kwa biashara ya dawa za kulevya.
Kuhusu kuteketeza dawa za kulevya kama Bangi, Heroine na Cocaine amesema uteketezaji wa dawa hizo uko kwa mujibu wa sheria ambayo inaeleza jinsi ya kuziteketeza huku akitumia nafasi hiyo kueleza umuhimu wa waandishi wa habari kushirikiana na Mamlaka hiyo kuendelea kushirikiana kutoa elimu kwa umma ili kukomesha dawa za kulevya.