Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mtoto wa miaka 12 amlawiti mtoto wa miaka 10

Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe linamshikilia mtoto mwenye umri wa miaka 12 kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wa darasa la nne mwenye umri wa miaka 10 katika moja ya shule ya msingi iliyopo halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe.

Kamishna Msaidizi wa Polisi mkoa wa Njombe ACP. Mahamoud Hassan Banga, amesema tukio hilo limetokea Aprili 4,2024 na kueleza kuwa Mwanafunzi huyo alikuwa akilawitiwa kwa ahadi ya kupewa fedha na Mtuhumiwa ambaye aliacha shule akiwa darasa la sita.

ACP Banga ameongeza kuwa kutokana na sheria ya Mtoto, Mtuhumiwa huyo ameachiwa kwa dhamana wakati jeshi la polisi likiendelea na upelelezi na kufafanua kuwa pindi utakapokamilika taratibu za kisheria zitafuatwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *