Mkurugenzi wa huduma za Afya Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais – TAMISEMI Dkt.Rashid Mfaume amebaini ukiukwaji wa mununuzi ya vifaa ikiwemo majokofu ya kuhifadia damu katika kituo cha afya Mwalugulu katika Halmashauri ya Msalala Mkoa Shinyanga.
Dkt. Rashid Mfaume amebaini changamoto hizo akiwa katika ukaguzi na ziara ya usimamizi shirikishi wa shughuli za huduma za Afya ndani ya mwalugulu health Centre.
Dkt. Mfaume amebaini majokofu mawili yaliyonunuliwa katika kituo hicho kwaajili ya kuhifadhi damu kuwa ni majokofu kwaajili ya matumizi ya nyumbani.
Aidha pia alibaini kuwa baadhi ya vifaa tiba ikiwemo mashine ya dawa za usingizi (Anaesthetic Machine) vimepokelewa bila kukaguliwa ilihali malipo yalikwisha fanyika bila viambatanisho vya taarifa ya ukaguzi na mapokeo.