Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Miili sita ya wanafunzi wa shule ya  Ghati  Memorial waliokufa maji yaopolewa

Idadi ya watoto waliofariki kutokana na gari walilikuwa wamepanda kusombwa na maji imefikia sita baada ya miili mingine kupatikana kutokana na juhudi za uokozi zinazoendelea.


Awali iliripotiwa kuwa mtoto mmoja amefariki na wengine saba kutojulikana walipo baada ya gari la Shule ya Ghati Memorial School kusombwa na maji alfajiri ya leo wakati wakijaribu kuvuka korongo la Engosengiu kata ya Sinoni mkoani Arusha.


Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo alifika katika eneo la ajali na kulaumu uzembe wa dereva uliosababisha vifo vya watoto hao na wengine kutojulikana walipo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *