Watu Watatu wamefariki na wengine Zaidi ya 300 wamejeruhiwa katika Mtaa wa Embakasi Jijini Nairobi baada ya mtambo wa Gesi kulipuka usiku wa kuamkia leo Februari 2, 2024 .
Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limesema Watu 271 wamepelekwa kwenye Vituo vya Afya na wengine 27 walifanyiwa vipimo zaidi katika eneo la tukio ambapo baada ya mlipuko watu wengi walisikika wakipiga kelele na kukimbia kila mahali kwa kuhofia milipuko Zaidi.
Msemaji wa Serikali, Isaac Mwaura amesema tukio hilo limetokea katika kiwanda cha gesi cha Kentainers Company Ltd kilichopo karibu na makazi ya watu.