Channel ya kanisa la kanisa kuu la muhubiri wa Nigeria marehemu TB Joshua,’Emmanuel TV’ imefungiwa na mtandao wa YouTube, kwa kile kinachotajwa kukiuka sera zake za matamshi.
Hali hii inakuja ikiwa ni wiki kadhaa baada ya uchunguzi wa BBC na OpenDemocracy kubainisha taarifa za unyanyasaji wa kingono na mateso yaliyokuwa yakifanywa na kiongozi huyo wa kanisa.
TB Joshua alifariki mwaka 2021, ambapoi Kanisa lake la Synagogue Church of All Nations (Scoan) sasa linaongozwa na mkewe Evelyn Joshua.