Njiwa aliyekamatwa akihisiwa ni jasusi aachiwa huru

Polisi Nchini India wamemuachilia njiwa aliyehisiwa kuwa jasusi wa China baada ya kuzuiliwa kwa miezi minane na kumwachia porini Jumanne, shirika la habari la Press Trust of India liliripoti.

Mateso ya njiwa huyo yalianza mwezi wa Mei alipokamatwa karibu na bandari huko Mumbai akiwa amefungwa pete mbili miguuni, zikiwa na maneno yaliyofanana na ya Kichina.

Polisi walihisi kuwa Njiwa huyo anahusika katika ujasusi na kumchukua, baadaye wakampeleka katika Hospitali ya Wanyama ya Bai Sakarbai ya Bai Sakarbai Dinshaw Petit.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *