Mkongwe wa WWE afunga ndoa na binti wa miaka 45

Bingwa wa mchezo wa mieleka kutoka WWE, Hulk Hogan (70) amefunga ndoa kwa mara nyingine tena huko Mjini Florida, nchini Marekani na mrembo Sky Daily (45).

Kwa mujibu wa watu wa karibu na Hulk, wanasema kuwa mrembo Sky amebadilisha Maisha ya mshikaji wao, amekuwa mtu wa furaha muda mwingi tofauti na hapo awali na ndoa yao haikuwa ya mambo mengi kiukweli ni ndoa ya kifamilia zaidi.
Hii ni ndoa ya tatu kwa Hulk ambaye anawatoto wawili kutoka kwenye ndoa yake ya kwanza na ndoa ya pili hakupata mtoto na hii ni ya tatu kwa mrembo Sky ambaye ni mwalimu wa Yoga, mwenye watoto watatu.

da

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *