Mil. 30 kukarabati Kanisa lilovamiwa na kuvunjwa

Hayo yamebainishwa na Paroko wa Parokia Hiyo Padri Deodatus Vedasto wakati akizungumza na Jambo Fm baada ya Misa Takatifu iliyofanyika chini ya miti nje ya kanisa hilo huku wakinyeshewa na mvua, ambapo amesema vifaa vilivyo haribiwa vina thamani ya zaidi ya milioni 2.6 ambapo ukarabati mpya wa kanisa hilo utagharimu zaidi ya milioni 30 huku akiwaomba wadau pamoja na waumini wa kanisa hilo kuwaunga mkono.

Baada ya Jambo Fm kuripoti tukio la watu wasiofahamika kuvamia na kuvunja ukuta wa Kanisa Katoliki Parokia Ya Nyakato-Buzirayombo Jimbo Katoliki La Rulenge – Ngara Wilaya Ya Chato Mkoani Geita, kanisa hilo limelazimika kufanyiwa ukarabati upya ambao utagharimu zaidi ya milioni 30 kutokana na unajisi uliofanyika ndani ya kanisa hilo.

Baadhi ya waumini wa kanisa hilo waliojitokeza kushiriki misa Takatifu iliyofanyika chini ya mti wamejitokeza kuanza kuchimba msingi ili kuanza ukarabati wa kanisa hilo na kusema tukio lililofanyika ndani ya kanisa ni kufuru hivyo watashiriki kikamilifu ili kanisa hilo litakatifuzwe upya ili waweze kuabudia ndani ya kanisa hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *