Wananchi hawana uwelewa wa Kodi Huduma

Licha ya kupanda kwa kiwango cha ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri ya Manispaa Ya Shinyanga na uwepo wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kutumia fedha za mapato ya ndani, halmashauri hiyo bado inakabiliwa na changamoto ya ukusanyaji mapato hususani kodi ya huduma (Service Levy).

Mstahiki Meya Wa Manispaa Ya Shinyanga Eliasi Ramadhan Masumbuko wakati akizungumza na Jambo Fm ofisini kwake na kubainisha kwamba halmashauri hiyo imekuwa ikichukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya vikao vya mara kwa mara na wafanyabiashara.

Uchunguzi uliofanywa na Jambo Fm kupitia maoni yaliyotolewa na ya baadhi ya wakazi wa manispaa ya shinyanga kuhusiana na uelewa wao juu ya kodi mbalimbali zinazotozwa na serikali umegundua kuwa wananchi hao hawana uelewa wa kutosha kuhusu kodi hizo.

Kupitia mapato ya ndani Manispaa Ya Shinyanga imetekeleza na inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa masoko ya kisasa uliohusisha soko kuu kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 1.8, uboreshwaji wa miundombinu ya barabara na maeneo ya kupumzikia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *