Mwanza kutanua Uwanja wa Ndege

Serikali ina Mkakakati wa kuufanya uwanja wa Ndege wa Mwanza kuwa wa Kimataifa kwa kujenga Miundombinu ya Kisasa likiwemo jengo la Abiria ambapo tayari zaidi ya Bilioni 11 zipo kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi huo.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza CPA Amos Makalla, Amebainisha hayo mapema leo tarehe 13 Septemba, 2023 wakati wa Kikao na watumishi wa Uwanja wa Ndege Mwanza ambapo ameagiza pia Mamlaka ya Uwanja wa Ndege kuandaa michoro ya jengo la Abiria, upanuzi, Hoteli na Shopping Mall ili kuleta unadhifu kwenye huduma.

Katika uboreshaji huo Makalla amewataka Mamlaka ya viwanja vya ndege kuendelea na shughuli mbalimbali kama ujenzi wa Jengo la abiria la Kisasa huku akibainisha kuwa hawapaswi kusubiri tena kwani limekua likichelewa kujengwa na Serikali ya Rais Samia imeamua kuboresha uwanja huo kuwa wa kimataifa.

Makalla amesema Shughuli za mamlaka ya viwanja vya ndege pamoja na jeshi la anga kwenye eneo hilo hazipaswi kuingiliwa na wananchi waliovamia na kwamba serikali ipo kwenye uboreshaji wa uwanja huo kuwa wa kimataifa ndio maana kuna shughuli mbalimbali zinaendelea.

Mkuu huyo wa Mkoa amefafanua kuwa Serikali inaandaa utaratibu wa kuwaondoa wananchi zaidi ya Elfu Moja (Nyumba 800) wa Mitaa ya Mhonze, Kihili na Bukyanhulu waliovamia eneo la Mamlaka ya Uwanja wa ndege ili kutoa fursa kwa shughuli za Uwanja kufanyika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *