Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mgogoro wa mpaka kati ya Geita na Shinyanga waanza upya

Mgogoro wa mpaka katika eneo lenye madini la Mwakitolyo unazidi kufukuta kwani eneo hilo linagombewa na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga na halimashuri ya wilaya ya Nyan’gwale huku baraza la madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga wakiitaka serikali kuangalia upya utatuzi wa mgogoro huo.

Wakizungumzia mgogoro huo katika baraza la madiwani baadhi ya madiwani katika halimashuri ya Wilaya ya Shinyanga wamesema wanashangazwa kuona eneo hilo lenye utajiri wa madini liinatambulika kuwa lipo Nyangwale wakati katika suala la upigaji kura katika chaguzi zote wananchi wa eneo hilo ushiriki katika halimashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Awali akitoa majibu juu ya suala hilo katibu tawala msaidizi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga upande wa Serikali za Mitaa, Abraham Makana amesema kwa mujibu wa mipaka na mgawanyo wa maeneo kiserikali eneo hilo linatammbulika kuwa lipo katika halimashauri ya wilaya ya Nyangwale Mkoani Geita.

Naye makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Nicodemus Samsoni ameiomba Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kuingilia kati mgogoro huo kwani unaleta usumbufu kwa wakazi wa maeneo hayo kwani mpaka sasa hawafahamu kama wao ni sehemu ya halimashuri ya Shinyanga au Nyang’wale Mkoani Geita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *