Staa wa muziki kutoka Nigeria, Teni, amefunguka kuwa mwezi Julai wakati anarekodi albamu yake ya pili iitwayo ‘‘Tears of the Sun’’ aligundulika kuwa na maambukizi ya koo ambayo yangeweza kukatisha kipaji chake cha kuimba.
“Baada ya kupoteza sauti kwa muda, madaktari wangu walinishauri nifanyiwe upasuaji mkubwa au niwe tayari kupoteza sauti yangu,…baada ya upasuaji mwezi Oktoba 2023, nilirejesha sauti yangu. Hatimaye Novemba hii nimerejea kwenye kazi yangu na nina ngoma mpya inaitwa ‘Malaika’ ni wimbo wangu wa sifa na shukrani kwa Mungu kwa rehema na neema zake kwangu,” ameandika mrembo huyo Instagram.
