MFAHAMU MWANDISHI NA MTANGAZAJI ALIYETEULIWA KUWA WAZIRI MKUU MPYA BURKINA FASO.

Rimtalba jean emmanuel ouédraogo waziri mkuu mpya wa burkina faso ni mzaliwa wa ouagadougou au wagadugu ambao ni mji mkuu wa burkina faso, Amekua mwandishi wa habari na mtangazaji  wa burkina faso na baadae kuwa mwanasiasa.

Amekua waziri wa mawasiliano, utamaduni, sanaa na utalii kuanzia oktoba 25, 2022 hadi desemba 6, 2024, ambapo disemba 7 2024 ameteuliwa kuwa waziri mkuu mpya wa burkina faso.

Mnamo septemba 2022 rimtalba jean emmanuel, alitangazaza kujiunga na ujio wa vuguvugu la kizalendo la kulinda na kurejesha amani ii lililoitwa patriotic for safeguard and restoration (mpsr) ambapo jeshi lilijitangazia kuwa liko madarakani.

Rimtalba jean emmanuel ouédraogo amesoma ouagadougou. Katika chuo kikuu cha joseph-ki-zerbo, alijiandikisha katika idara ya sosholojia. Alifaulu mtihani wa ushindani wa taasisi ya habari na mawasiliano sayansi na mbinu (istic), alioupata mwaka 2006. Amekua mshauri katika sayansi na mbinu za habari na mawasiliano ana shahada ya sosholojia na shahada ya uzamili katika upatanishi na usimamizi wa migogoro. Alikuwa mhariri mkuu kisha mkurugenzi wa shirika la utangazaji wa televisheni la burkina faso (rtb) kutoka 2016 hadi 2021.

Rimtalba jean emmanuel ouédraogo alianza kuingia kwenye siasa, mnamo oktoba 25, 2022 alipoteuliwa kuwa waziri wa mawasiliano, utamaduni, sanaa na utalii na pia msemaji wa serikali ya mpito iliyoongozwa na apollinaire joachim kyélem de tambèla kutoka 2022 mnamo 2024.

Akiwa waziri, alitia saini uamuzi wa kusimamisha radio france internationale nchini burkina faso mwaka wa 2022 na wakati wa mabadiliko ya mawaziri ya desemba 17, 2023 alipandishwa cheo na kuwa waziri wa nchi na baada ya kuvunjwa kwa serikali ya burkinabè mnamo desemba 6, 2024, ameteuliwa kuwa waziri mkuu wa burkina faso kuanzia desemba 7, 2024.




Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *