Kwa mujibu wa mtandao wa CCN umesema kuwa Mwanamke anayejulikana kama Jane Doe, anadai akiwa na umri wa miaka 13 (mwaka 2000) alibakwa na P. Didy Pamoja na Jay Z kwenye sherehe baada ya Tuzo za Video Music mwaka 2000.
Mwanamke huyo anasema alianza kuhisi kizunguzungu baada ya kunywa kinywaji kwenye sherehe hiyo na akaingia kwenye chumba cha kulala kilicho karibu. Anadai Carter ‘Jay Z’ alimbaka kwanza akifuatiwa na Combs ‘P Didy’ . Mwanamke huyo anasema alimchapa kibao P Didy na kukimbia kutoka kwenye sherehe hiyo, kulingana na mashtaka yaliyorekebishwa.
Kesi hiyo ilifunguliwa awali dhidi ya Didy mnamo mwezi Oktoba, lakini Jumapili iliyopita mwanamke huyo alimuongeza Shawn Carter ambaye ni rapa na mfanyabiashara anayejulikana kama Jay-Z kama mshtakiwa katika kesi ya madai.
Ikumbukwe Jay Z ndiye mtu mashuhuri wa kwanza kutajwa kwenye madai ya unyanyasaji wa kingono yanayomhusisha Didy, Katika taarifa aliyoitoa kwa CNN, Carter ‘Jay Z’ aliziita tuhuma hizo za kikatili sana kiasi kwamba anawashi wafungue kesi ya jinai, si ya madai! Yeyote atakayefanya uhalifu kama huo dhidi ya mtoto mdogo anapaswa kufungwa, sivyo?” – Jay Z
Didy alishtakiwa kwa makosa ya ulanguzi wa ngono, njama ya uhalifu, na mashtaka yanayohusiana na ukahaba ingawa alikana mashtaka hayo na amekataa madai yote katika takriban kesi 30 za madai zilizowasilishwa dhidi yake.
Katika majibu yake kwa CNN Jumapili yaliyoelekezwa kwa wakili wa Doe, Jay Z alidai ombi la upatanishi lilikuwa “jaribio la kutaka hongo.” Pia alisema wakili huyo, “ambaye nimefanya utafiti kidogo kumhusu, anaonekana kuwa na tabia ya aina hii ya maigizo!” – Jay Z