NDEGE ILIYOKUA IKIELEKEA URUSI YAANGUKA, WATU 38 WAFARIKI DUNIA….

Ndege ya Shirika la Ndege la Azerbaijan iliyokuwa imebeba jumla ya watu 67 imeanguka karibu na mji wa Aktau uliopo nchini Kazakhstan na kusababisha vifo vya watu 38 waliokuwa ndani, kwa mujibu wa taarifa za Mamlaka ya Kazakhstan.

Kwenye operesheni kubwa ya uokoaji, manusura 29 wakiwemo watoto wawili waliokolewa kutoka kwenye mabaki ya ndege hiyo, Naibu Waziri Mkuu wa Kazakhstan, Kanat Bozumbayev ameongeza kwa kusema kuwa watu 11 wako katika hali mbaya zaidi.

Ndege ya Azerbaijan Airlines, safari ya J2-8243, ilikuwa ikisafiri kutoka mji mkuu wa Azerbaijan, Baku, kuelekea Grozny katika eneo la Chechnya nchini Urusi kabla ya kutua kwa dharura umbali wa takribani kilomita 3 (maili 1.8) kutoka Aktau, taarifa ya shirika hilo la ndege lilisema.

Picha za eneo la ajali zilionyesha wakati manusura waliokuwa wameduwaa walipojitokeza kutoka kwenye mabaki ya ndege iliyokua imeteketea. 

Manusura wote wamepelekwa hospitalini, mamlaka za Kazakhstan zilisema mapema. Hakuna kati ya manusura walio raia wa Kazakhstan, alisema Naibu Waziri Mkuu.

“Miili iko katika hali mbaya, imeungua sana, yote imekusanywa,” Bozumbayev alisema. “Sasa itakuwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti, na utambuzi utafanyika.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *