Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Matumizi ya dawa za macho zisizo rasmi yanaweza kupelekea upofu usiotibika

Serikali kupitia Wizara ya Afya imewaasa wananchi kuacha tabia ya kutumia dawa za macho kwa lengo la kutibu ugonjwa wa Red Eyes zisizo rasmi kwa kuwa matumizi hayo yanaweza kupelekea upofu usiotibika kama ambavyo itakuwa kwa wengi wa wagonjwa waliokwisha kupata madhara kwenye kioo cha jicho kwa kutumia vitu hivyo.

Wito huo umetokewa leo Februari 8, 2024 na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya Prof. Paschal Ruggajo alipokua anaongea na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar Es Salaam.

Amesema, Baadhi ya vitu vinavyotumika ni pamoja na dawa zene vichocheo vya ‘steroids’ ambazo wananchi wanakwenda kununua wenyewe kwenye maduka ya dawa, tangawizi, chai ya rangi illiyokolea majani, mafuta tete yaliyokuwa yakitumika wakati wa janga la Covid – 19, maji ya chumvi na maziwa ya mama, ambavyo vitu vyote hivyo sio salama na havijaelekezwa na wataalamu.

Aidha, Prof. Ruggajo amesema hadi sasa takwimu zinaonesha ongezeko la kuenea kwa ugonjwa huu ambapo jumla ya wagoniwa 12,332 wameonwa katika vituo vyetu vya tiba na wagonjwa hawa wameonwa katika Mikoa 23 ya Tanzania Bara.



Mikoa inayoongoza kwa ugonjwa huo ni Dar es Salaam ambapo idadi ya wagonjwa imefikia 6,412, Pwani wagonjwa 4,041, Dodoma 363, Morogoro 307, Mtwara 193, Shinyanga 193, Tanga 190, Lindi 101.” Amesema Prof. Ruggajo.


Wizara inaendelea kusisitiza jamii kuzuia kuenea kwa maambukizi haya kwa kuzingatia usafi binafsi na kanuni za Afya ikiwa ni pamoja na Usafi wa mikono na uso, Kuzuia kugusa macho yako kadri uwezavyo, Nawa mikono na maji tiririka na sabuni au na tumia vipukusi mara kwa mara, zingatia kutokushikana mikono maeneo ya sehemu za ibada, Tumia taulo au leso za karatasi kufuta tongotongo au machozi, Fika Kwenye kituo cha kutolea huduma mara upatapo dalili hizi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *