Jambo La Leo

Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mashahidi 7 watoa ushahidi kesi ya ugaidi

Mahakama kuu ya Tanzania divisheni ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi masjala ya Shinyanga imetupilia mbali mapingamizi ya upande wa utetezi dhidi ya Jamhuri katika ushahidi wa maelezo ya onyo ya shahidi wa 7 katika kesi ya uhujumu uchumi na ugaidi no 3 ya mwaka 2023.

Jaji wa mahakama hiyo Jaji Geofrey Isaya amesema baada ya kupitia maelezo ya pande zote mbili na kupitia vifungu vyote vya sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai amesema Jamhuri ilifuata utaratibu wote uliopaswa kuchukuliwa na kuna kifungu kilichokiukwa wakati wa uchukuaji na uandikaji wa maelezo ya onyo kwa mtuhumiwa vilizingatiwa.
Katika hatua nyingine Jaji Isaya amesema baada ya kupitia mapingamizi hayo moja ya pingamizi ni la mshitakiwa kusema kuwa alipigwa na kunyanyaswa ili kuweza kuandika maelezo ya onyo ambapo amesema itafunguliwa shauri dogo ndani ya shauri kubwa ili kusikiliza na kubaini namna alivyofanyiwa mshitakiwa huyo kabla ya kuandika maelezo.

Jaji Isaya amehairisha shauri hilo mapema leo hadi hapo litakapopangwa tena ili kuendelea kusikilizwa ambapo tayari mashahidi 7 wamesikilizwa ushahidi wao huku washtakiwa hao wakirudishwa mahabusu.

Kesi hiyo uhujumu uchumi na ugaidi no 3 ya mwaka 2023 imesikilizwa mfululizo katika mahakama kuu ya tanzania divishen ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi masjala ya Shinyanga hiyo mbele ya jaji Geofrey Isaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *