Mwanamke huko nchini Nigeria-Abuja, anayetambulika kama Effie Keens Osano, amemzawadia Nancy ambaye ni dada wa kazi za nyumbani hati ya nyumba ambayo itakuwa yake.
Mbali na nyumba pia amemzawadia pesa taslimu, simu janja na simu nyingine ya kwa ajili ya mama yake, pamoja na mkoba kama kuthamini kile ambacho amekuwa akifanya kwake kwa kuhudumu muda wa miaka 10 kwake na miaka miwili ambayo alikuwa likizo mbali na famiala yake ambapo amekuwa mlezi bora kwa watoto wake.