Marufuku wanafunzi kubebwa gari zisizokaguliwa

Jeshi la polisi Mkoani Shinyanga limepiga marufuku wanafunzi kubebwa na magari ambayo hajakaguliwa ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza ikiwemo ajali, ambapo magari mawili kati ya 40 yaliyokaguliwa leo yameng’olewa namba za usajili kutokana na ubovu huku wamiliki wake wakielekezwa kuyarekebisha na kuendelea na kazi.

Marufuku hiyo imepigwa na Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani mkoani Shinyanga SSP Wenzeslaus Gumha baaada ya ukaguzi wa magari hayo uliofanyika katika karakana ya polisi mkoani humo ambapo imebainika baadhi ya shule hazijafikisha magari yanayobeba wanafunzi wao kwa ajili ya ukaguzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *